ADVERTS

LOGO

Search This Blog

Thursday, September 20, 2012

PRESENTER AND DJ SEARCH ARUSHA!





Hapa ni siku  mbili kabla ya shindano ambapo washiriki wote walikuwa katika studio za radio 5 wakijifunza mabo mbali mbali.....


SIKU YA SHOW




Hawa ni baadhi ya washiriki wa shindano la Radio 5 Presenter search  wakijifua kabla ya kuanza kwa mchujo wa awali.....




Maandalizi yalikuwa yakiendelea kwa washiriki waliokuwa wakielekezwa namna ya kutumia studio ndogo na mzee wa mwongozo...Willy  Cosmas...Huku Goodluck  Kisanga na Dj King Davy wakiongoza maandalizi ya burudani.
Jimmy Mtemi meneja wa Radio 5 akizungumza  na wageni wakati wa ufunguzi
Huyu ni Dj King akifanya mambo kidigitali zaidi
Mama Afrika kulia..Mzee Estomih Malla(chief Judge) na Ones Mo,...ndio waliokuwa wakiongoza panel ya majaji.
Upande mwingine kulikuwa na Erick Lupiana sambamba na meneja wa Tripple A  Bori.
Mwangaza jummanne na Tonie Kaisoi, Semio Sonyo wakiwa na mgeni wao Mr C kutoka  Mj Fm....
Hawa ni baadhi ya washiriki wakiwa makini kufuatilia shindano...



Burudani ilikuwa sehemu ya shindano na hapa jamaa anajulikana  kama Shuba Akishambulia Jukwaa.


Friday, September 7, 2012

NI KAWAIDA KWETU KUTEMBELEWA NA WAGENI

 Wanamuziki wa Kalunde Band hapa ni Bob Rudala na deo mwana mbilimbi wakiwa katika viwanja vya radio 5
 Meneja masoko wa Radio 5 Sarah  Lazaro(katikati) akiwa na Deo mwanambilimbi na  Bob rudala


 Huyu ndiye Deo Mwanambilimbi mwenye jezi ya Tanzania akiwa na Meneja masoko wa Radio 5.
 Sarah Lazaro akiwa na Bob Rudala aliyewahi kutamba na sjingo ya nimekuchagua wewe.
 David Rwenyagira akiwa na Bob rudala na Deo mwanambilimbi.
 Program Manager Philip Magese akiwa na Bob rudala na Deo mwanambilimbi.
 Clara Moita akiwa na Deo Mwanambilimbi na Bob Rudala.


Tuesday, August 21, 2012

WAZIRI MKUU ETHIOPIA AFARIKI

Waziri mkuu wa Ethiopia Meles Zenawi Amefaariki dunia asbuhi ya leo akiwa na umri wa miaka 57.Aliyekuwa naibu wake ndiye atakayekaimu nafasi hiyo....Endelea kusikilza radio 5fm kwa taarifa zaidi na kufatilia blog hii kwa historia ya zenawi.

Friday, August 10, 2012

RADIO 5 YASHINDA NANE NANE KASKAZINI

 Katika maonesho ya wakulima yaliyofikia  kilele  tarehe  nane mwezi wa nane zilishiriki taasisi   nyingi...lakini radio 5 iliibuka mshindi kwa taasisi zote za binafsi na serikali zilizoshiriki....Pichani wafanyakazi wakiwa na kombe mara baada ya kutangazwa washindi na waziri mkuu Mh.Mizengo Pinda.
 Charles  Mayomi akiweka mitambo sawa wakati wa shuhuli za ufunguzi wa sherehe hizo.

 Mara baada ya kutangazwa washindi...Pichani ni David Rwenyagira akiwa habarisha Live wanannchi juu ya kilichokuwa kinaendelea huko themi.
Wafanyakazi wa radio 5wakiwa na kombe la ushindi kutoka kushoto ni  Deo    G,Tonnie Kaisoi,Pili Sirikwa ,Sarah Lazaro,Semio Sonyo,Ashura Mohamed,Charles Mayomi na David Rwenyagira
Semio Sonyo akitangaza  wakati wa maonesho hayo.

Wednesday, June 20, 2012

MUBARAKA HOI

Taarifa za kutatanisha zimeibuka kuhusu afya ya Hosni Mubarak aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano ya kutaka mageuzi nchini Misri mwaka jana.
Baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa uhai wake unasitiriwa kwa kutumia mashine baada ya kuhamishwa kutoka gerezani hadi kwenye hospitali ya kijeshi mjini Cairo.
Hosni Mubarak
Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela
Mubarak mwenye umri wa miaka 84 aliugua kiharusi akiwa jela, hali iliosababisha ahamishwe hadi hospitalini akiwa mahututi.
Kiongozi huyo aliondolewa mamlakani mwaka jana kufuatia maandamano ya raia wa nchi hiyo yakupinga utawala wake.
Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuamrisha mauaji ya baadhi ya waandamanaji hao.
Mara kadhaa kumekuwepo na taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya rais huyo wa zamani lakini kila mara zimepuuzwa.
Taarifa hizo kuhusu afya yake zimetokea wakati ambapo maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwenye bustani ya Tahrir kulaani uamuzi wa baraza la kijeshi wa kujilimbikizia mamlaka.