Taarifa za kutatanisha zimeibuka kuhusu afya ya Hosni
Mubarak aliyeondolewa madarakani kufuatia maandamano ya kutaka mageuzi
nchini Misri mwaka jana.
Baadhi ya vyombo vya habari vimetangaza kuwa
uhai wake unasitiriwa kwa kutumia mashine baada ya kuhamishwa kutoka
gerezani hadi kwenye hospitali ya kijeshi mjini Cairo.Kiongozi huyo aliondolewa mamlakani mwaka jana kufuatia maandamano ya raia wa nchi hiyo yakupinga utawala wake.
Mwezi uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuamrisha mauaji ya baadhi ya waandamanaji hao.
Mara kadhaa kumekuwepo na taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya rais huyo wa zamani lakini kila mara zimepuuzwa.
Taarifa hizo kuhusu afya yake zimetokea wakati ambapo maelfu ya waandamanaji wamekusanyika kwenye bustani ya Tahrir kulaani uamuzi wa baraza la kijeshi wa kujilimbikizia mamlaka.